October 5, 2022

Tutalipiza Iwapo Urusi Itatumia Silaha za Kemikali, Rais Biden Aapa

0 0
Read Time:2 Minute, 21 Second
50 100

Rais wa Marekani Joe Biden amesema Nato “itajibu” ikiwa Urusi itatumia silaha za kemikali nchini Ukraine.

Rais – ambaye yuko Ulaya kwa mazungumzo na washirika – hakuelezea nini inaweza kumaanisha.

Maoni yake yalikuja katika siku ambayo haijawahi kushuhudiwa katika mikutano ya dharura mjini Brussels, ambapo viongozi wa nchi za Magharibi walionyesha msimamo mmoja dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Bw Biden anasafiri kuelekea Poland siku ya Ijumaa ambapo zaidi ya raia milioni mbili wa Ukraine wamekimbia kutoka kwa mapigano.

Alipoulizwa kama matumizi ya silaha za kemikali na Vladimir Putin wa Urusi yangechochea jibu la kijeshi kutoka kwa Nato, Bw Biden alijibu kwamba “itasababisha jibu kwa namna fulani”.

“Tungejibu ikiwa ataitumia. Asili ya mwitikio itategemea aina ya matumizi,” alisema.

Mataifa ya Magharibi yameonya kuwa Urusi inaweza kujiandaa kutumia silaha za kemikali au za kibaolojia nchini Ukraine, huku uvamizi wake nchini humo ukiingia wiki yake ya tano.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema itakuwa “janga” ikiwa Bw Putin atatumia silaha za kemikali, wakati Katibu Mkuu wa Nato Jens Stoltenberg ameweka wazi kuwa itasababisha madhara makubwa.

Ikulu ya White House imeunda timu ya usalama ya taifa kuangalia jinsi Marekani na washirika wanapaswa kuitikia iwapo Urusi itaanzisha mashambulizi ya kemikali. Lakini hakuna pendekezo Nato ingejibu kwa kutumia silaha za kemikali, anasema Mhariri wa BBC wa Marekani Sarah Smith.

Bwana Biden hapo awali alisisitiza Marekani na Nato haitatuma wanajeshi wake Ukraine kwa hofu ya makabiliano ya kijeshi ya moja kwa moja na Urusi.

Rais alikuwa akizungumza baada ya mkutano wa dharura wa viongozi wa Nato kujadili jinsi ya kukabiliana na uwezekano wa matumizi ya silaha za maangamizi, pamoja na msaada wa kijeshi kwa Ukraine na vikwazo vikali zaidi dhidi ya Moscow.

“Jambo moja muhimu zaidi ni sisi kukaa kwa umoja,” rais alisema baada ya mkutano huo.

Bw Biden anatarajiwa kutangaza makubaliano makubwa na Umoja wa Ulaya kuhusu gesi asilia iliyosafishwa, katika jaribio la kupunguza utegemezi wa Ulaya kwa nishati ya Urusi.

Makubaliano hayo yangeifanya Washington kuipatia EU angalau mita za ujazo bilioni 15 za ziada za mafuta ifikapo mwisho wa mwaka.

Vikundi vinne vipya vya vita vya Nato vinatumwa Hungary, Slovakia, Romania na Bulgaria.

Rais pia alisema ataunga mkono wito wa kutimuliwa kwa Urusi kutoka kundi la mataifa tajiri G20. Lakini alisema hilo litategemea maoni ya wanachama wengine.

Baada ya mkutano na Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen mjini Brussels Ijumaa asubuhi, Bw Biden ataelekea Poland. Rais atasafiri hadi mji wa Rszeszów, karibu na mpaka na Ukraine, ambapo atakutana na wakimbizi wa Ukraine.

Bw Biden ametangaza kuwa Marekani itapokea hadi raia 100,000 wa Ukraine na kutoa nyongeza ya $1bn (£756m) katika chakula, dawa, maji na vifaa vingine.

Zaidi ya wakimbizi milioni 3.6 wameikimbia Ukraine tangu uvamizi huo uanze, wakiwemo zaidi ya milioni 2.1 kwenda Poland.

Bw Biden pia atawatembelea wanajeshi wa Marekani ambao wametumwa huko hivi majuzi.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %