September 27, 2022

Viongozi wa Jubilee Katika Jimbo la Nyandarua Wakiongozwa n Sicily Kariuki Waomba Amani

0 0
Read Time:1 Minute, 2 Second
37 100

Baadhi ya wawaniaji chini ya chama cha Jubilee katika kaunti ya Nyandarua wametoa wito kwa wakenya na wanasiasa wengine kukumbatia amani na utangamano.

Pia wamewataka viongozi kuepusha kauli na matukio yanayoweza kusababisha uvunjifu wa amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu.

Wawaniaji hao, wakiongozwa na aliyekuwa Katibu wa Baraza la Mawaziri la Maji na Umwagiliaji Sicily Kariuki wako tayari kueneza chama katika eneo hilo.

Wakizungumza wakiwa kwenye kampeni katika vituo mbalimbali ndani ya Jimbo la Ndaragwa, wagombea hao walieleza dhamira yao ya kukiimarisha chama hicho na pia kuhakikisha kinanyakua viti vingi katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Agosti.

Kariuki anajiweka katika nafasi nzuri ya kunyakua kiti cha Ugavana wa Nyandarua, ambacho kwa sasa kinashikiliwa na Gavana Francis Kimemia. Wawili hao wanatazamia kura za mchujo za chama kuona ni nani atakayebeba bendera ya Chama cha Jubilee kabla ya uchaguzi huo.

 Kariuki aliandamana na aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Kitaifa ya Uangalizi wa Polisi John Waiganjo ambaye anawania Kiti cha Seneta kaunti hiyo na Sasha Wamae, anayewania nafasi ya Mwakilishi wa Wanawake Kaunti.

Viongozi hao wawaniaji waliahidi kuhakikisha kuwa chama cha Jubilee kinakuwa chama maarufu zaidi katika eneo hilo, huku wakijitolea kuhubiri amani na kuepukana na matamshi yatakayozua mizozo, hata joto la kisiasa likiendelea kupanda.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %