October 3, 2022

Mwili wa Polisi Aliyepotea Wapatikana

0 0
Read Time:48 Second
53 100

Mwili wa afisa wa polisi aliyekuwa amepotea katika eneo la Chesuman kwenye bonde la Kerio, kaunti ndogo ya Marakwet Magharibi, kaunti ya Elgeyo Marakwet umepatikana.

 Akithibitisha hilo Ofisa Mkuu wa Marakwet Magharibi Bosita Omukolongolo amesema kuwa afisa huyo alikuwa amepotea tangu tarehe 5 mwezi huu ambapo mwili wake ulipatikana na wanafunzi wa shule ya msingi ya Chesuman kilomita 2 kutoka kwenye shule hiyo.

Omukolongolo alisema kuwa alipokea simu kutoka kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo kuwa wanafunzi wake ambao walikuwa wanatafuta kuni walipata mwili wa afisa huyo ambao ulikuwa umeoza, tukio ambalo iliwalazimu maafisa wa polisi katika eneo hilo kufika sehemu hio ili wachukue hatua ya kuondoa mwili wa afisa huyo.

Vile vile Omukolongolo amesema kuwa inashukiwa kuwa afisa huyo alipoteza maisha yake kwa kunyongwa kwa vile mwili wake haukuwa na alama yoyote.

Chanzo kilichompelekea afisa huyo apoteze maisha yake bado hakijajulikana huku uchunguzi ukianzishwa

Mwili wa afisa huyo ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya rufaa mjini Iten. 

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %